Watu saba wafariki kufuatia ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru

  • | K24 Video
    44 views

    Watu saba wakiwemo watoto wawili wamefariki mapema leo kufuatia ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru. Ajali hiyo iliyohusisha matatu mbili aina ya Nissan na trela iliyokwama ilitokea karibu na kituo cha kibiashara cha Kikopey Gilgil. Waliopata majeraha wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali tofauti eneo hilo.