Watu saba wanahofiwa kufariki kwenye mafuriko Makueni

  • | Citizen TV
    2,840 views

    Watu saba wanahofiwa kufariki baada ya kusombwa na maji kaunti ya Makueni. Juhudi za kutafuta miili ya waliosombwa na maji katika Mto Muooni ulioko eneo la Mukaa zinaendelea. kufikia sasa miili mitatu imepatikana. Zoezi la kutafuta miili hiyo zinaendeshwa na maafisa wa shirika la msalaba mwekundu na idara ya kukabiliana na mikasa ya kaunti ya Makueni.