Watu waliohudhuria Tamasha la Muziki la Israeli wakikimbia wakati shambulizi linaendelea

  • | VOA Swahili
    650 views
    Shambulizi katika tamasha la muziki wa Tribe of Nova lililofanyika uwanjani inaaminika lilikuwa baya sana kwa mauaji ya raia katika historia ya Israeli, huku watu wasiopungua 260 wamefariki na bado idadi haijajulikana ya wale waliochukuliwa mateka. Darzeni ya wanamgambo ambao walivuka kinyume cha sheria kwenye uzio imara unaotenganisha pande mbili waliwapiga risasi vijana waliokuwa katika burudani waliokusanyika kwa ajili ya usiku wa furaha wa muziki wa kielektroniki kusherehekea sikukuu ya Kiyahudi ya Sukkot. Idadi isiyojulikana ya watu waliokuwepo katika tamasha hilo walitekwa nyara na hawajulikani waliko. Hamas inadai kuwa inawashikilia zaidi ya Waisraeli 100 kama mateka. - AP #israel #gaza #reels #igreels #videography#voa #hamas #hostages