Watu wanne wafariki baada ya kubugia pombe

  • | Citizen TV
    871 views

    watu wanne wamefariki na wengine saba kulazwa hospitalini mwingi kaskazini, kaunti ya kitui, baada ya kunywa pombe haramu. Inaarifiwa kuwa Watu hao walianza kulalamikia kuhisi joto jingi mwilini, kuumwa na kichwa na kuharisha baada ya kubugia pombe hiyo inayojulikana kama " kaluvu". Muuzaji wa pombe hiyo ni miongoni mwa wanaotibiwa katika hospitali ya mwingi level 4. manusura wanashuku huwa huenda pombe hiyo ilikuwa na sumu kwani sio mara yao ya kwanza kunywa pombe wanayonunua kwa mhudumu huyo.