Watu wanne wafariki baada ya kusombwa na maji katika jiji la Nairobi usiku wa kuamkia leo

  • | K24 Video
    229 views

    Watu wanne walifariki baada ya kusombwa na maji katika jiji la Nairobi usiku wa kuamkia leo kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. mmoja wao alikuwa ni afisa wa polisi aliyefariki alipokuwa katika shughuli ya kuwaokoa watu wanne waliokwama kwenye maduka yao katika kituo cha basi cha country bus baada ya maji kufurika. serikali ya kaunti ya nairobi imetangaza mikakati ya kukabiliana na mafuriko na kuwapa msaada walioathirika.