Watu wanne wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Pokot Magharibi

  • | KBC Video
    24 views

    Watu wanne wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka huko Turkwel, Kaunti ya Pokot Magharibi mapema leo alfajiri. Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Pokot Magharibi Abdullahi Jire Mohamed alithibitisha mkasa huo na kusema kuwa mgodi huo umefungwa kwa muda usiojulikana. Aliongeza kuwa uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha mkasa huo uliotokea saa tisa alfajiri. Haya yanajiri takriban saa 48 baada ya wakaazi kulalamikia kufungwa kwa migodi hiyo huku kukiwa na wasiwasi kutoka kwa viongozi wa eneo hilo kuhusu athari za kimazingira na usalama wa wachimbaji madini. Ben Chumba anatuarifu zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive