Watu wanne wauawa Bangale, Tana River

  • | KBC Video
    61 views

    Watu wanne akiwemo mvulana wa umri wa miaka mitano wameuawa kwenye makabiliano ya kijamii katika eneo la Elnigha, kaunti ndogo ya Bangale, kaunti ya Tana River. Wakazi wanasema tukio hilo lilichochewa na kukamatwa kwa wanaume wawili walioshukiwa kuhusika kwenye kisa cha ubakaji. Wakazi wamehimizwa kudumisha amani huku polisi wakiahidi kuwachukulia hatua waliohusika na mauaji hayo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive