Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mbolea ya ruzuku kaunti ya Trans-Nzoia

  • | Citizen TV
    248 views

    Wakulima katika kaunti ya Trans-Nzoia wanaitaka serikali kuwakamata wafanyibiashara walaghai wanaotatiza mpango wa mbolea ya ruzuku kwa kujilimbikizia mbolea hiyo na kisha kusababisha uhaba. Suala hilo limepelekea mbolea hiyo kuuzwa kwa bei ya juu katika maduka ya kibinafsi huku baadhi ya wafanyibiashara wakibadilisha mbolea kutoka kwenye magunia ya NCPB ili kuiuza bei ghali.