Watu watatu wanusurika kifo kaunti ya Embu baada ya gari lao kutumbukia majini

  • | KBC Video
    141 views

    Watu watatu wamenusrika kifo baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto Ena,katika barabara yenye shughuli nyingi ya Embu-Meru,katika kaunti ya Embu.Dereva wa lori hilo lililokumbwa na mkasa,lililokuwa ikisafirisha saruji alikuwa akijaribu kukwepa kugonga lori jingine lililoingia ghafla barabarani, wakati ajali hiyo ilipotokea.Walioathirika wamepelekwa katika hospitali ya Tenri Ena kwa matibabu.