Watu wawili waliuawa katika eneo la nyakach

  • | Citizen TV
    4,070 views

    Hali imesalia tete katika mpaka wa kaunti za Kisumu na Kericho, ambako watu 2 walifariki na wengine 5 wakijeruhiwa kufuatia makabiliano yaliyozuka eneo la Nyakach. Kwa mujibu wa polisi, machafuko hayo yaliyoanza jana mchana yalichochewa na wizi wa mifugo, iliyosababisha makundi ya vijana kutoka kaunti hizo mbili kukabiliana na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.