- 15,035 viewsDuration: 1:30Watu wawili wamepigwa risasi na kufariki katika mji wa Nanyuki uliopo katikati ya Kenya, wakati wa maandamano dhidi ya mpango wa Marekani wa kuanzisha kituo cha kuwaweka wagonjwa wa Ebola katika kambi ya kijeshi iliyo karibu. Mmoja wa wahanga alipigwa risasi katika eneo lililo karibu na Kambi ya Ndege ya Laikipia ambapo maandamano yalikuwa yanaendelea na alifariki baada ya kupelekwa hospitalini na mwingine alikuwa tayari amefariki alipofikishwa hospitalini na askari. Caro Robi anaelezea zaidi #bbcswahili #ebola #kenya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw