Watu zaidi wakamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya Ojwang'

  • | Citizen TV
    14,571 views

    Afisa mkuu wa polisi kituo cha central Samson Talam amekamatwa kwa madai ya kuhusika na kifo cha mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang'. Talam alikamatwa alasiri ya leo na maafisa wa kitengo cha kuchunguza malalamishi dhidi ya polisi na kufikishwa katika ofisi za mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi (IPOA) inayochunguza kifo cha ojwang'. Talam alikamatwa saa chache baada ya raia mmoja kukamatwa kwa kosa la kufuta kanda ya CCTV katika stesheni ya central na kudaiwa kulipwa shilingi 3,000. Haya yalijiri huku afisa mwingine wa polisi james mukhwana aliyekamatwa alhamisi akifikishwa mahakamani.