Watu zaidi ya watano wamefariki kufuatia mzozo wa maeneo ya kuchimba migodi huko Marsabit

  • | Citizen TV
    826 views

    Zaidi ya watu watano wamethibitishwa kufariki katika eneo la Illo kaunti ya Marsabit kufuatia mzozo wa maeneo ya kuchimba migodi. Taharuki imeendelea kutanda huku wakazi wakihama maeneo hayo kwa kuhofia usalama wao. Migodi ya Illo katika eneo la Dabel imevutia zaidi ya watu 30,000 wa kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo Meru, Migori na hata nchi jirani ya Ethopia, wakipiga kambi kutafuta riziki.