Watumbukia kwenye maji ya barafu kuadhimisha mwaka mpya Tokyo

  • | BBC Swahili
    1,041 views
    Waumini wa kanisa moja mjini Tokyo wameukaribisha mwaka mpya kwa kuoga maji ya barafu katika utamaduni wa kila mwaka ambao ulianza miaka 68 iliyopita. Wanaume huvaa nguo kiunoni na wanawake gauni nyeupe kabla ya kutumbukia ndani ya maji yaliyojaa vipande vya barafu. Ibada ya Shinto inasemekana kutakasa nafsi na kuleta afya njema katika mwaka mpya. #bbcswahili #tokyo #tamaduni