Wauguzi sasa wanaonya kwamba kuna uhaba wa wahudumu nchini, swala ambalo linazidi kuathiri huduma za matibabu nchini.
Akizungumza mjini Machakos wakati wa maadhimisho ya wiki ya wauguzi, Rais wa muungano wa wauguzi nchini Collins Otieno, anasema baraza la magavana limezembea katika kuidhinisha kuajiriwa kwa wauguzi ilhali wanaofuzu kila mwaka nchini ni zaidi ya wauguzi elfu kumi. Muungano huo unaitaka serikali kutekeleza mkataba wa maelewano wa mwaka wa 2017 na kuwapandisha ngazi wauguzi ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu.Otieno pia anasema kuwa taasisi za kutoa mafunzo kwa wauguzi zimejaa na huenda walio na ndoto ya kujiunga na kmtc wakakosa kufanya hivyo katika miaka miwili ijayo.