Wauzaji vitabu wataka wahusishwe katika mabadiliko

  • | K24 Video
    23 views

    Huku wauzaji wa vitabu wakijiandaa kwa biashara yao kunoga kabla ya kufunguliwa kwa shule mwezi wa Januari, wameiomba serikali kuwashirikisha katika mijadala kuhusu mabadiliko katika mitaala wa CBC. Kulingana nao, wamo katika hatari ya kupata hasara kufuatia uamuzi wa serikali wa kuunganisha baadhi ya masomo, wakati wachapishaji na wauzaji vitabu tayari walikuwa wameagiza vitabu.