Wauzaji wa pombe ya mnazi walalamikia kuhangaishwa na polisi

  • | K24 Video
    125 views

    Wakaazi wa kaunti ya kilifi wamelalamika kuhusu msako dhidi ya kinywaji cha mnazi wakiitetea kuwa si kileo haramu ila ni ya asili na ina manufaa ya kijamii. Wauzaji pia wamesema kuwa wananyanyaswa na maafisa wa polisi na kulazimika kulipa shilingi elfu mbili kabla ya kuachiliwa. akiapa kuutetea uuzaji wam pombe ya mnazi, spika wa kaunti ya bunge la Kilifi Teddy Mwambire amesema iwapo wauzaji watazidi kukandamizwa kwa kuuza kinywaji hicho kwa njia ya halali basi wakaazi wataandamana. na katika kaunti ya Bungoma kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Francis Kooli amelaumu bodi inayopeana leseni za kuendesha biashara ya pombe nchini kwa kuwa shughuli hiyo imesababisha kikwazo katika vita dhidhi ya pombe haramu.