Wavuvi eneo la Bonje waendeleza juhudi za upandaji mikoko kurejesha hali ya misitu kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    177 views

    Makundi ya wavuvi wanaotegemea bahari katika eneo la Bonje eneobunge la Kinango kaunti ya Kwale wanaendeleza juhudi za upandaji mikoko ili kurejesha hali ya misitu hiyo ya bahari. Hii ni baada ya sehemu hizo kuharibiwa na hali ya anga na utumizi mbaya wa miti hiyo na wenyeji. Juhudi hizo zinalenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sawa na kuimarisha bishara ya hewa ya Kaboni.