Wazazi na walimu wa kijiji cha Shikomari, Navakholo waungana kuboresha elimu eneo hilo

  • | Citizen TV
    420 views

    Wazazi katika kijiji cha shikomari eneo bunge la navakholo wametakiwa kuchukulia masomo ya wanao kwa makini na kuhakikisha wanafika shuleni kila siku ili kutimiza azma ya serikali ya asilimia100 ya wanafunzi kujiunga na shule. Wakizungumza katika shule ya msingi ya Shikomari eneo bunge la Navakholo kaunti ya kakamega, walimu ambao walisoma katika shule hiyo wakiongozwa na Joel Shilingi wamesikitikia idadi ya wanafunzi wanaofika shuleni eneo bunge hilo wakiwataka wazazi kujukumika na kuhakikisha kuwa wanao wanapata elimu ili kukomesha visa vya utovu wa usalama eneo hilo.