Wazazi wahimizwa kutowaficha watoto walemavu

  • | Citizen TV
    170 views

    Wiki chache baada ya kupitishwa kwa Mswada wa Haki za walemavu wa 2025, kundi la wakurugenzi wanawake kutoka sekta mbalimbali kaunti ya Trans Nzoia, wamezuru shule za watoto wenye mahitaji maalum, wakihimiza wazazi kutowaficha watoto wao bali wawape elimu ili waishi maisha ya heshima na kujitegemea. Wakizungumza katika Shule ya Wasiosikia ya St Columbus mjini Kitale baada ya kutoa misaada ya chakula, sabuni, beseni, sare na SODO, viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kumaliza unyanyapaa na ukatili dhidi ya watoto wenye ulemavu. Mwalimu mkuu wa shule hiyo ameelezea furaha yake kwa msaada huo, huku padri wa Kanisa Katoliki akiwasihi wazazi kuwajumuisha watoto wao katika maisha ya kawaida