Wazazi waikashifu serikali kuhusu ufunguzi wa shule

  • | Citizen TV
    1,898 views

    Mamia ya Wanafunzi mapema leo walikwama katika vituo tofauti vya magari ya usafiri wa umma, baada ya wizara ya elimu kuahirisha ghafla ufunguzi wa shule. Wazazi waliojawa na ghadhabu wakiilaumu serikali kwa uamuzi wake wa kuchelewa licha ya kufahamishwa kuhusu utabiri wa hali ya anga. Haya yanajiri huku wizara ya Elimu ikiwaagiza wakuu wa shule kuhakikisha wanafunzi waliofika shuleni wanasalia.