Wazazi waishi kwa hofu kufuatia visa vya wizi wa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano Eldoret

  • | K24 Video
    169 views

    Wazazi katika mtaa wa Langas jijini Eldoret wanaishi kwa hofu kufuatia msururu wa visa vya wizi wa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano katika siku za hivi majuzi. Mwaka wa 2024 umeshuhudia watoto zaidi ya kumi wakiripotiwa kutoweka katka mazingira ya kutatanisha na mpaka leo hawajulikani waliko. licha ya kilio cha wenyeji, idara za uslama zimekosa majibu ya wanaohusika na wizi huo ambao wakazi wa Langasa wanaamini ni mtandao wa ulanguzi wa watoto .