Wazazi wapiga kambi nje ya shule ya Hillside Endarasha huku wakitaka kujua hatma ya wanao

  • | Citizen TV
    1,868 views

    Mamia ya wazazi kutoka shule ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri sasa wanazishutumu asasi mbali mbali kuhusu mkondo wa uchunguzi wa mkasa wa moto ambao umesababisha vifo vya wanafunzi 17. Baadhi ya wazazi waliokusanyika nje ya shule hiyo, wanadai kuwa hawajapata ripoti kamili kuhusu hali ya wana wao kwani hawajaruhusiwa kuingia shuleni humo.