Wazee wa jamii ya Busia washauriwa kuimarisha 'korti' za nyumbani

  • | West TV
    36 views
    Idara ya mahakama katika kaunti ya busia inawahamasisha wazee wa jamii mbali mbali katika kaunti hiyo kuhusu njia mbadala za kutatua migogoro ya kijamii na kesi ndogo ndogo kama njia moja ya kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani katika kaunti hiyo. Idara hiyo imefichua hayo wakati wa uhamasisho kwa umma kuhusu idara hiyo mjini busia.