Wazee wa Kaya wafanya matambiko kinango

  • | Citizen TV
    207 views

    Wazee wa Kaya eneo la Kinango kaunti ya Kwale wamefanya matambiko ya kuhamisha madhabahu ya Kaya Mavyonini ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa bwawa la Mwache. Wazee hao wanaamini matambiko hayo ya kuhamisha madhabahu yataondoa mikosi na balaa zinazoweza kujitokeza iwapo itasalia hapo.Matambiko hayo yalifanywa kwa nyimbo za kitamaduni na kuchinjwa kwa ng'ombe wawili weusi, kondoo mmoja mweusi, mbuzi wawili weusi na kuku mmoja.