Wazee wa kijiji wachukua jukumu la kuwaadhibu wahalifu baada ya serikali kutotuma chifu

  • | Citizen TV
    1,461 views

    Hebu tafakari, kijiji kisichokuwa na viongozi wa utawala kama chifu au naibu wake ila wakazi wanachukua hatua ya kudumisha amani na nidhamu. Katika kijiji cha Mosora kaunti ya Kisii, ukipatikana na kosa la wizi unafukuzwa pamoja na familia yako kupitia kikao maalum cha wanakijiji kabla ya kuruhusiwa baadaye kujitetea. Mwanahabari wetu Chrispine Otieno alihudhuria moja kati ya vikao hivyo maalum na hii hapa taarifa yake.