- 1,711 viewsDuration: 3:27Wazee wa jamii za Mlima Kenya Mashariki wameapa kumuunga mkono Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki katika safari yake ya kuendelea kuwa Naibu Rais na hatimaye kuwa Rais baada ya mihula miwili ya Rais William Ruto. Wakizungumza katika kongamano la wazee Kaunti ya Embu, wazee hao wamewataka wakazi wa Mlima Kenya Magharibi kumuunga mkono Kindiki kama walivyomuunga mkono aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na marais wastaafu.