Waziri Ezekiel Machogu asema alinukuliwa vibaya kuhusu ufadhili wa vyuo vikuu

  • | Citizen TV
    358 views

    Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amekanusha hoja kuwa alisema serikali haitafadhili vyuo vikuu. Kulingana naye, alinukuliwa vibaya kwani tayari serikali imeshatenga shilingi bilioni 50 kwa vyuo vikuu vya umma. Hata hivyo, waziri Machogu amevitaka vyuo vikuu kubuni mbinu za kujitafutia mapato zaidi badala ya kutegemea ufadhili wa serikali pekee.