Waziri Justin Muturi ampa Rais Ruto onyo kali, akimtaka akomeshe visa vya utekaji nyara

  • | K24 Video
    5,525 views

    Waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi amempa Rais William Ruto onyo kali, akimtaka achukue hatua mara moja kukomesha visa vya utekaji nyara na mauaji kinyume cha sheria nchini kenya. akizungumza katika chumba cha kuhifadhia maiti cha city jijini Nairobi baada ya kupatikana kwa miiili miwili ya vijana waliokuwa wametekwa nyara Mlolongo mwezi jana, Muturi alisisitiza kuwa kipaumbele cha serikali ni kuhakikisha wananchi. Waziri muturi amekosoa hadharani namna serikali inavyoshughulikia masuala ya usalama, hatua inayodhihirisha migawanyiko inayozidi kujitokeza ndani ya serikali na wasiwasi wa umma juu ya hali ya usalama nchini.