Waziri Kindiki aagiza kuhamishwa kwa maafisa wa KRA, KEBS na Uhamiaji eneo la Isebania

  • | Citizen TV
    1,094 views

    Waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki ameagiza kuhamishwa kwa maafisa wote wa polisi, maafisa wa KRA, wale wa kukadiria ubora wa bidhaa na wanaojihusisha na kudhibiti bidhaa ghushi katika mpaka wa Isebania. Hatua hiyo imejiri baada ya watu watano kuuwawa kwa kupigwa risasi kufuatia makabiliano kati ya wakazi na maafisa wa polisi. Waziri Kindiki ameongoza mkutano wa usalama eneo la Isebania. Aidha Kindiki amesema kuwa serikali haitaendelea kuwahamisha maafisa wanaokosa nidhamu bali itawafuta kazi. Hata hivyo Kindiki amewakosoa wakazi kwa kuvamia kituo cha polisi cha Isebania. Aidha wanasiasa waliochochea vurugu watashtakiwa.