Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki

  • | Citizen TV
    1,363 views

    Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa ameaga dunia, akipokea matibabu jijini Dar Es Salaam. Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa na makamu wa rais wa Tanzania Daktari Philip Mpango. Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa la Tanzania, Mpango amesema kuwa Lowassa amefariki katika taasisi ya matibabu ya moyo ya Jakaya Kikwete. Lowassa alihudumu kama waziri mkuu wa Tanzania chini ya rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, kuanzia 2005 hadi 2008 . Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kuanzia hii leo.