Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu ahudhuria maziko ya mtoto wa waziri wake

  • | VOA Swahili
    1,750 views
    Maziko ya mtoto wa kiume wa waziri katika serikali ya Israeli na mkuu wa jeshi wa zamani Gadi Eizenkot, aliyeuawa katika mapigano huko Ukanda wa Gaza yamefanyika Ijumaa huko kaskazini mwa Tel Aviv. Gal Meir Eizenkot, umri miaka 25, alikuwa ni komando anayepigana katika eneo la kaskazini ambako majeshi ya Israeli yanapambana na Hamas katika wilaya chache wanazo zishikilia, baada ya Israel kuuteka mji wa Gaza City mwezi uliopita. Alikuwa kati ya maelfu ya wanajeshi wa akiba walioitwa kuendesha mashambulizi kujibu mauaji ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 na utekaji nyara uliofanywa na Hamas, kikundi cha Kiislam cha Palestina kinacho tawala Ukanda wa Gaza. Hamas ilisema kijana huyo aliuawa na bomu lililokuwa limewekwa katika handaki la waasi katika wilaya ya Tal al-Zaatar. - Reuters .#Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu #maziko