Waziri Murkomen asema wandani wa Charles Ong’ondo Were walihusika kwa mauaji yake

  • | Citizen TV
    3,970 views

    Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amesema kwamba uchunguzi kuhusu mauaji ya mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were, umebainisha kwamba baadhi ya waliohusika kwenye shambulizi hilo ni wandani wake. Akizungumza kwenye mkutano maalum wa Jukwaa La Usalama unaoangazia hali ya usalama katika kaunti ya Meru, waziri Murkomen amesema kwamba serikali inafanya kila iwezalo kuwahakikishia wananchi wote usalama.