- 365 viewsDuration: 3:11Rais William Ruto ametangaza kuwa mpito wa gredi ya 10 umefikia asilimia tisini na tisa na kwamba juhudi za kuhakikisha wanafunzi wote wanajiunga na Gredi ya 10 zinaendelea. Hayo yakijiri Waziri wa elimu Migos Ogamba amewaonya walimu wakuu wa shule za upili dhidi ya kukataa kuwasajili kwa mitihani ya kitaifa wanafunzi ambao hawajamaliza kulipa karo. Akizungumza alipoandamana na rais huko Nandi, Ogamba amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya walimu watakaopatikana wakifanya hivyo.