- 45 viewsWaziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku amewaonya watumishi wa umma wanaochelewa kufiika kazini kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Akizungumza baada ya kufanya ziara ya ghafla katika afisi kuu ya Kamishina wa eneo la Kaskazini Mashariki, Waziri Ruku alitamaushwa na idadi ndogo ya wafanyikazi waliokuwa wamefika kazini kufikia saa mbili ya asubuhi. Waziri huyo aliahidi kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa maafisa wa serikali unatiliwa maanani.