- 3,074 viewsDuration: 4:02Waziri wa afya Aden Duale naye pia amethibitisha namna serikali ilivyohusika katika kutanzua mvutano kuhusu Nairobi Hospital. Hata hivyo, akizungumza mjini Mombasa, Duale ametoa hakikisho kuwa hospitali hiyo inasalia ya kibinafsi na serikali tu imekuwa ikisaidia kulainisha huduma katika hospitali hiyo kubwa ya kibinafsi nchini.