Waziri wa afya asema Wakenya watalipa 2.75% ya mishahara kwenye mpango mpya wa SHIF

  • | Citizen TV
    1,745 views

    Waziri wa afya Susan Nakhumicha sasa anasema kuwa, ada ya hazina ya bima ya matibabu ya afya ya jamii huenda ikasalia asilimia 2.75 ya mshahara wa mfanyakazi kama ilivyopendekezwa. Akizungumza kaunti ya Trans Nzoia, Waziri Nakhumicha amesema kuwa, japo wanasubiri maamuzi ya mahakama, hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kila mkenya anapata huduma kupitia hazina ya SHIF. Haya yanajiri huku utata ukiendelea kugubika malipo ya wagonjwa kupitia NHIF