Waziri wa afya Dkt. Deborah Mlongo Barasa atangaza kuongeza kwa malipo kwa SHA

  • | Citizen TV
    437 views

    Wizara ya afya imetangaza mabadiliko katika bima ya afya ya SHA. Waziri wa afya Deborah Barasa amesema serikali imeongeza malipo yatakayotolewa kwa wagonjwa waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa wanaohitaji huduma za ICU na HDU. Fedha hizo zikiongezwa kutoka shilingi 4,600 hadi shilingi elfu 28.....Mbali na hayo malipo ya huduma za matibabu kwa wanaougua saratani yameongezwa kutoka shilingi laki 4 hadi elfu 550 kwa kila familia ili kusaidia wanaoathirika. Tangu kuzinduliwa kwa mfumo wa SHA miezi mitano iliyopita, changamoto nyingi zimeripotiwa, ila Waziri akisema serikali inaweka juhudi za kuhakikisha maswala yaliyoibuka yanatatuliwa..