Waziri wa ardhi Alice Wahome asema makato ya ushuru wa nyumba sharti yalipwe

  • | Citizen TV
    1,803 views

    Utata umeendelea kugubika mdahalo wa ushuru wa nyumba huku sasa Waziri wa ujenzi na nyumba Alice Wahome sasa akiwatahadharisha waajiri dhidi ya kusitisha malipo hayo. Waziri Wahome anasema kuwa kukubaliwa kwa ombi la serikali la kuendelea kukusanya pesa hizo hadi tarehe kumi mwezi januari, waajiriwa wote sharti wawasilishe makato ya mishahara kama ilivyo ada. haya yanajiri huku Viongozi wa vyama vya Wafanyikazi nchini wakitoa onyo kwa Waajiri dhidi ya kujumuisha ushuru wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwenye mishahara.