Waziri wa mambo ya nje wa Marekani akutana na rais wa Palestina

  • | VOA Swahili
    332 views
    - - - - - Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas Ijumaa asubuhi katika mji mkuu wa Jordan, Amman. Blinken ameianza siku yake ya pili ya ziara ya kidiplomasia huko Mashariki ya Kati, akilenga kuzima mzozo ulioenea wa kikanda huku akiahidi uungaji mkono kamili kwa Israeli wakati inapokabiliana na kundi la Hamas na kujiandaa kwa uvamizi wa ardhini unaotarajiwa katika Ukanda wa Gaza.