Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza aeleza sababu za kusitishwa ufadhili Gaza

  • | VOA Swahili
    351 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron aliwasili Jumatano katika ghala la polisi mpakani Bulgaria karibu na Uwanja wa Ndege wa Sofia, ambako polisi wa Bulgaria wanahifadhi maboti yaliokusudiwa kutumika katika uvukaji mpaka haramu kupitia lango la English Channel ambapo polisi wa Bulgaria waliyakamata kwa msaada wa Uingereza. Wakati akijibu swali kuhusu kusitishwa ufadhili Gaza, Cameron aeleza: “Tunacho taka kufikia ni uhakika kamili kuwa hili halitatokea tena. Inabidi tuweke wazi hapa, kuwa inavyoelekea ni kana kwamba kulikuwa na watu wanaofanya kazi [katika shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia misaada kaskazini mwa Gaza], UNRWA, ambao walishiriki katika shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel. Hili halikubaliki. Ndiyo maana tulisitisha ufadhili wetu, na ndiyo maana uchunguzi huu unafanyika. Tunataka ufanyike kwa haraka, kwa sababu kuna wafanyakazi wengi wa UNRWA wanaofanya kazi muhimu kabisa ndani ya Gaza, ambako ndiyo mtandao pekee wa kusambaza misaada, kuhakikisha tunawafikishia misaada watu wanaouhitaji kwa dharura ya hali ya juu." #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran #davidcameron #bulgaria