Waziri wa Uchukuzi aahidi paa mpya katika uwanja wa JKIA kwa muda wa wiki

  • | Citizen TV
    5,140 views

    Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen sasa ameahidi kuwa paa za kisasa zitawekwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika muda wa juma moja lijalo. Hii ni baada ya sehemu za uwanja huo kuonyeshwa zikivuja kufuatia mvua iliyonyesha jijini Nairobi. Murkomen aliyezuru uwanja huo pia amelaumu ukosefu wa miundo msingi ya kupitia maji kuwa sababu ya kufurika kwa sehemu za uwanja huu baada ya mvua kubwa kunyesha.