Waziri wa usalama awaonya wezi wa mifugo

  • | Citizen TV
    825 views

    Waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki amewaonya wezi wa mifugo wanaowahangaisha wakaazi wa Igembe Kaskazini kaunti ya Meru. Waziri Kindiki pia akiwaonya wanasiasa wanaoshirikiana na wezi hao wa mifugo akisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Alikuwa akizungumza kaunti ya Meru ambako ameahidi kuajiriwa kwa polisi wa akiba 140 kuimarisha usalama eneo la Igembe North ambako kumeshuhudiwa visa vya wizi wa mifugo.