Waziri wa usalama Kindiki azuru kaunti ya Turkana kuzindua kaunti ndogo ya Lokichogio

  • | Citizen TV
    179 views

    Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof Kithure Kindiki yuko kaunti ya Turkana kuzindua kaunti ndogo ya Lokichogio na kumteua naibu kamishna wa kwanza wa Lokichogio. Kaunti ndogo ya Lokichogio imefikisha nane, idadi ya kaunti ndogo katika kaunti ya Turkana. Waziri Kindiki amesema serikali itazidi kubuni kaunti ndogo ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi na kuboresha usalama mashinani. Aidha, waziri ametangaza kuwa serikali itaongeza idadi ya polisi wa akiba ili washirikiane na vitengo vya usalama kuwakabili wahalifu, haswa wezi wa mifugo na magaidi.