Waziri wa usalama Kithure Kindiki azuru Transmara kutathmini machafuko ya mzozo wa mpaka

  • | Citizen TV
    357 views

    Waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki anazuru Transmara Magharibi leo kutathmini hali ya usalama kufuatia machafuko yaliyochochewa na mzozo wa mpaka wa Enoreteet na Nkararo. Ziara ya Kindiki inajiri wakati ambapo uhasama unazidi kutokota baina ya Jamii ya Isiria na Irwa Shinkishu eneo hilo.