Weego yatoa hamasisho kwa wakenya kuhusu usalama barabarani

  • | Citizen TV
    295 views

    Kampuni ya teksi za mitandaoni ya Weego imewarai wakenya kuwa waangalifu barabarani, ili kupunga ajali za barabarani. Weego iliyoshiriki hafla ya Park and Vibe huko Kirigiti kaunti ya Kiambu, imewaomba madereva wake zaidi ya elfu kumi nchini, kuepuka vileo wanapoingia Barabarani. Wamesisitiza haja ya watu kujikuza kiuchumi kwa madereva na wanaomiliki magari. Mamia ya biashara zilishiriki hafla hio inayonuia kuzipa biashara ndogo, nafasi ya kupenya kwenye masoko ya bidhaa wanazouza.