Wetangula awataka mahasibu kushiriki katika mchakato wa kuandaa bajeti na maswala ya uchumi

  • | K24 Video
    25 views

    Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula amewataka mahasibu nchini kushiriki katika mchakato wa kuandaa bajeti na maswala ya kuboresha uchumi ili kuafikia maendeleo na kukabiliana na mfumuko wa bei za bidhaa nchini. Akizungumza mombasa katika kongamano la 41 la mahasibu nchini, ICPAK - Wetangula amesema mchango wa mahasibu katika kamati mbalimbali za bunge ikiwemo kamati ya bajeti ni muhimu katika kuafikia makadirio ya bajeti yatakayoimarisha uchumi wa taifa