Will Perry: 'Nimechoka kuchekwa kila siku'

  • | BBC Swahili
    Will Perry ni muogeleaji aliyewakilisha Uingereza katika michezo ya Olimpiki ya walemavu ,anasema "amechoka’’ kuchekelewa kwa sababu ya kimo chake kifupi. Anakabiliwa na hali inayojulikana kama achondroplasia na anasema watu kama yeye mara nyingi huchukuliwa video au kudhihakiwa mtaani. Perry mwenye umri wa miaka 21 anatoa wito kwa watu kuwawajibisha wale wanaofanya hivyo. @BBC News Swahili #ulemavu #michezo #afya