Wito watolewa kwa wenyeji wa Garissa kuwachagua wanawake kwenye kura

  • | Citizen TV
    180 views

    Wito umetolewa kwa wenyeji wa kaunti ya Garissa kuwachagua wanawake katika uchaguzi mkuu ujao kwa nia ya kubadili mkondo wa kisiasa kwa jamii ya wafugaji ambayo haitambui uongozi wa wanawake. Katika mkutano ulioandaliwa na shirika moja lisilo la kiserikali la Eco Africa na kuleta pamoja wazee wa jamii hiyo, vijana na viongozi wanawake, ilibainika Kwa changamoto kubwa kwa kina mama kutoka maeneo ya wafugaji ni mila potovu inayowanyima nafasi katika uongozi ilhali wana uwezo wa kuongoza. Ukosefu wa elimu ya kutosha na hamasisho kuhusu haki zao za kidemokrasia pia yamechangia kuongeza vikwazo kwa wanawake wanaojitosa kwenye ulingo wa siasa.