Wizara inafanyia majaribu ya kimatibabu ya dawa ya saratani

  • | K24 Video
    40 views

    Katika takriban kila dakika ishirini, mkenya huaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani, na hivyo inamaana kuwa zaidi ya vifo 28,000 huripotiwa kila mwaka. Hii ni zaidi ya asilimia 50 ya visa vya saratani vinavyogunduliwa kila mwaka nchini Kenya. Kwa kushirikiana na wadau kama vile kampuni ya dawa ya Roche inayotengeneza dawa za kutibu saratani, wizara ya afya inakusudia kuhakikisha aina zote za ugonjwa wa saratani zinagunduliwa katika hatua za awali, kama mojawapo ya malengo yake kabla ya kongamano la saratani mnamo februari mwaka ujao..